1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanajeshi wa Uingereza auawa na bomu nchini Afghanistan

21 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CvZ6

KABUL:

Nchini Afghanistan, mwanajeshi mmoja wa Uingereza ameuawa na bomu lililotegwa kando mwa barabara katika maeneo ya kusini mwa nchi hiyo.Mwanajeshi huyo aliuawa baada ya gari, alimokuwa akisafia, kulipuliwa na bomu. Wanajeshi wengine wa NATO walijeruhiwa.Shambulio hilo limefanyika katika mji wa Qala, ambao ulichukuliwa tena mwezi jana na vikosi vya mseto wa majeshi ya Marekani, Uingereza na Afghanistan kutoka mikono ya wapiganaji wa Kitaliban.