1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwalimu wa Uingereza arejea kwao

4 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CWTg

LONDON.Gillian Gibbons mwalimu wa kike kutoka Uingereza ambaye aliachiwa huru kutoka kifungoni nchini Sudan hapo jana anatarajiwa kuwasili kwao asubuhi hii.

Mwalimu huyo ambaye alikuwa akifundisha nchini Sudan alihukumiwa na mahakama ya Sudan kifungo cha siku 15 baada ya kuwaruhusu wanafunzi wake kuiita sanamu ya dubwi jina la Mtume Mohammed SAW.

Kuachiwa kwake kutokana na juhudi za wabunge wawili waislamu wa Uingereza waliyokwenda Sudan ambapo jana walikuwa na mazungumzo na Rais Omar Hassan el Bashir.

Mara baada ya kuachiwa, mwanamke huyo aliwataka radhi waislam kwa kitendo hicho.