1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mvutano wa Marekani na China Mashambulizi ya mtandaoni

Oumilkheir Hamidou
13 Desemba 2016

Donlald Trump na kitisho cha kutoitambua "China Moja", mapigano ya kuukomboa mji wa pili kwa ukubwa wa Syria - Aleppo na jinsi demokrasia inavyohujumiwa kutokana na mashambulizi ya mtandaoni magazetini

https://p.dw.com/p/2UBoS
China Donald Trump auf Titelseite einer Zeitschrift
Picha: Getty Images/AFP/G. Baker

Tuanze lakini na kishindo kinachotishia kuitikisa siasa ya nje ya Marekani baada ya rais mteule wa Marekani Donald Trump kuuwekea suala la kuuliza mhimili wa uhusiano pamoja na jamhuri ya umma wa China ."Flensburger Tageblatt" linaandika: Kinachomshughulisha zaidi Trump sio Taiwan bali madaraka katika eneo la bahari ya Pacifik. Katika wakati ambapo Barack Obama alitegemea makubaliano ya biashara yanayojulikana kama "ushirikiano kati ya nchi zinazopakana na bahari ya Pacifik" ili kuinyamazisha China. Donald Trump anafuata mkakati mwengine. Anatafuta malumbano, ana washa moto na kupalilia. Peking, mfadhili mkubwa wa Marekani inayopigania kuwa dola kuu la kijeshi, haitovumilia kamwe hali hiyo. Kwa hivyo yadhihirika kana kwamba kasheshe itaendelea.

Mtaka yote hukosa yote

Gazeti la "Nordwest-Zeitung" linajiuliza kwanini Donald Trump anachochea ugonvi? Gazeti linaendelea kuandika: "Si kweli kwamba karata za Washington ndio zenye nguvu kuliko zile za Peking. Zaidi ya hayo viongozi wa serikali ya China-na hilo limedhihirika jumatatu, wako tayari kwa kila hali-kulipatia ufumbuzi suala la Taiwan lakini kwa masilahi yao wao. Sasa kilichompa Trump nini kwenda kuchokoa mambo katika eneo hilo? Ndo kusema ujinga wa mwanasiasa asiyekuwa na ujuzi wa kisiasa? Hasha. Tayari katika kampeni za uchaguzi, tajiri huyo mkubwa alitoa maneno makali dhidi ya China; na hata baadhi ya washauri wake wanasemekana ni watu waliopania kutafuta malumba na China. Wote hao wanabidi wautambue ule usemi "mtaka yote hukosa yote?

Vita havijamalizika Syria

Mapigano yamepamba moto katika mji wa pili kwa ukubwa wa Syria-Aleppo na vikosi vya serikali ya rais Bashar al Assad vinakaribia kushinda. Gazeti la "Neue Osnabrücker " linasema hata hivyo vita bado havijamalizika. "Ni ushindi kwa rais wa Syria, Bashar al Assad; akisaidiwa na washirika wake na hasa Urusi na Iran, amefanikiwa kuukomboa mji muhimu na wa pili kwa ukubwa nchini Syria-Aleppo. Haimaanishi lakini kwamba vita vimemalizika. Syria hata baada ya kukombolewa Aleppo, itasalia kuwa uwanja wa mapaigano. Wenye kutaka kuufumbua mzozo kwa mtutu wa bunduki wanajidanganya tuu, kinachoweza kutokea ni umwagaji damu usiokuwa na mwisho. Mazungumzo ya kisiasa yanaweza kurahisisha mambo, lakini kwa sasa yaonyesha kana kwamba hakuna anaevutiwa na fikra hiyo.

 Mashambulizi ya mtandaoni yatishia demokrasia.

Kinachoweza kushuhudiwa kampeni za uchaguzi mkuu zitakapoanza,si mzaha wa watoto watundu wanaopenda kuvuruga mambo mtandaoni. Ni kitisho cha kweli kilicholengwa kufuruga mfumo wa nchi za magharibi. Kwa maneno mengine "kuna hatari ya kuhujumuiwa mfumo wa demokrasia."Kampeni za uchaguzi mwaka 2017 zitakuwa tofauti kabisa na zilizopita. Huenda ukageuka kuwa mwaka wa kutupia lawama na kukana  na mengineyo. Changamoto kubwa inawakabili wanasiasa, vyombo vya habari na jamii kwa jumla.

 

Mwandishi:Hamidou Oumilkheir/Inlandspresse

Mhariri:Josephat Charo