1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mvutano wa kisiasa bungeni nchini Kenya

28 Aprili 2009

Vuta ni kuvute juu ya ni nani atakayekuwa mwenyekiti wa kamati ya shughuli za bunge na kiongozi rasmi wa shughuli za Serikali Bungeni imefika ukingoni hii leo.

https://p.dw.com/p/Hg17
Rais Mwai Kibaki wa KenyaPicha: AP/Presidential Press Services

Spika wa Bunge Bwana Keneth Marende ametoa uamuzi kwamba yeye binafsi ndiye atakayeshikilia wadhifa wa mwenyekiti wa kamati hiyo hadi Rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu Raila Odinga wanaoongoza serikali ya muungano watakaposhauriana na kwa kauli moja kumteua kiongozi rasmi wa shughuli za serikali bungeni.

Kwa maelezo zaidi ya taarifa hii mwandishi wetu Alfred Kiti kutoka Nairobi anatuarifu....


Mwandishi: Alfred Kiti
Mhariri: Mohamed Abdulrahman