1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mvutano mpya kati ya Urussi na Ukraine juu ya gesi wanukia

4 Machi 2008

-

https://p.dw.com/p/DHgS

KIEV

Rais wa Ukraine Viktor Yushchenko ameonya juu ya uwezekano wa kuanza upya vita vya gesi baada ya Urssi kukata usambazaji kwa asilimia 25 kwa nchi jirani.Kampuni pekee ya Gesi inayoendeshwa na serikali ya Urussi Gazprom imesema imechukua hatua ya kupunguza utoaji wa Gesi baada ya serikali ya mjini Kiev kushindwa kulipa deni la dollar millioni 600 madai ambayo Ukraine inayapinga vikali.Kampuni ya Gazprom ilisema kwamba usambazaji wa gesi kwenye nchi za Ulaya magharibi utaendelea kama kawaida.Umoja wa Ulaya umetoa mwito kwa pande hizo mbili Urussi na Ukraine kutafuta maafikiano juu ya mgogoro huo.Mwaka 2006 mvutano kama huo uliwahi kutokea na kutatiza usambazaji wa Gesi katika nchi za Umoja wa Ulaya.