1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mvua yaleta uharibu mkubwa

1 Januari 2008

---

https://p.dw.com/p/Cit2

LUSAKA

Zaidi ya watu 3000 kusini mwa Zambia wameachwa bila makazi baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko kufuatia mvua kubwa iliyonyesha.Nyumba nyingi zimeanguka au kusombwa baada ya mto uliokaribu na eneo hilo wa Magoye kufurika na kuvunja kingo na kuingia maeneo ya makaazi huko Mazabuka kiasi kilomita 150 kutoka mji mkuu Lusaka.Idara ya serikali inayohusika na majanga inajaribu kuwapa watu makaazi ya muda.Kamishna wa wilaya hiyo Misheck Chiinda amefahamisha kwamba mji wa kitalii ulioko eneo hilo la Kusini wa Siavonga umepoteza mawasiliano baada ya daraja pekee lililokuwa likiu-unganisha mji huo na miji mingine nchini Zambia kusombwa na mafuriko.Watalii wengi wanasemekana wamebakia katika hali ya kudangana kwenye eneo hilo.