1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mustakbali wa Yemen haujulikani bado

6 Juni 2011

Wananchi wa Yemen wafurahia kuondoka Abdalla Ali Saleh nchini.

https://p.dw.com/p/11VAb
epa02767478 Yemeni little girls flash 'victory signs' as they stand with anti-government protesters celebrating the departure of Yemeni President Ali Abdullah Saleh after four-month protests demand his ousting, in Sana'a, Yemen, 05 June 2011. According to media sources, thousands of Yemenis in several cities took to the streets in celebration, after President Ali Abdullah Saleh was announced to be in Saudi Arabia for treatment of wounds suffered two days earlier in an attack on his presidential palace. As President Ali Abdullah Saleh underwent a chest operation in Riyadh on 05 June, the protesters vowed to continue demonstrating until he and other officials are permanently removed from power. It is unclear whether Saleh, after four months of violent civil unrest and mass demonstrations calling for his ouster, intends to return to Yemen. EPA/YAHYA ARHAB +++(c) dpa - Bildfunk+++
Wasichana wa Ki-Yemeni wakionyesha "alama ya ushindi" kuondoka kwa Rais Abdullah Ali SalehPicha: picture alliance/dpa

Wananchi wa Yemen hadi saa hii wanasheherekea kile ambacho kinatarajiwa na watu wengi kuwa ni kuchomoza enzi mpya bila ya kuwa na Rais Abdullah Ali Saleh, ambaye hivi sasa anauguliwa nchini Saudi Arabia baada ya kufanyiwa operesheni mbili zilizofaulu za kutolewa marisawa ya kombora kifuani. Vyama vya upinzani nchini humo vimekula kiapo kwamba vitazuia kurejea nyumbani rais huyo.

Kamati ya vijana, ambayo imekuwa muhimu sana nyuma ya mapazia katika michafuko ya miezi mitatu iliopita ya kutaka kuuondosha utawala wa mabavu wa Abdullah Ali Saleh ilitoa mwito leo wa kuchukuliwa hatua za haraka kuhakikisha madaraka yanakabidhiwa kwa watu wengine. Ilizihimiza nguvu zote za kitaifa na kisiasa nchini Yemen kuanza kuunda baraza la mpito la urais. Kamati hiyo ilitaka iundwe serekali ya mabingwa kuongoza kipindi cha kujishikiza. Kikundi hicho cha vijana, waandalizi wa maandamano yaliokuwa yakifanyika karibu kila siku katika uwanja wa Sanaa tangu Februari, na ambayo yalikuwa yanaipinga serikali ya Abdullah Ali Saleh, kimewahimiza wananchi washeherekee kile walichokipongeza kuwa ni kupinduliwa Abdullah Ali Saleh. Maelfu ya watu walikwenda mabarabarani katika mji mkuu hapo jana kusheherekea kile walichokisema kuwa ni mwisho wa utawala wa Saleh. Mamia ya wengine walikwenda mabarabarani katika mji wa Taiz, wa pili kwa ukubwa huko Yemen. Watu hao walisema mapinduzi yamefikia lengo lake.

Upinzani bungeni Yemen umesema utatumia nguvu zake kuzuwia kurejea kwa nchini kwa Abdullah Ali Saleh, lakini msemaji wa chama tawala cha General People's Congress aliiambia televisheni ya Al-Arabiyya.

"Rais Abdullah Ali Saleh ni mzima, yuko Saudi Arabia ili afanyiwe uchunguzi, na atarejea kwa upesi kama iwezekanavyo. Taasisi za kikatiba zinaendelea kubakia pale pale. Jeshi linafanya kazi kwa utulivu, na pia chama tawala. Kwamba dola itasambaratika hiyo ni tu ndoto ya upinzani."

NO FLASH!!! epa02767113 An Anti-government protester hold a yemeni flag as he celebrates the departure of Yemeni President Ali Abdullah Saleh after four-month protests demand the ousting of Saleh_s 32-year regime, in Sana'a, Yemen, 05 June 2011. According to media sources, Yemeni President Ali Abdullah Saleh, hurt in a blast inside his compound, left Yemen for treatment in Saudi Arabia. EPA/YAHYA ARHAB +++(c) dpa - Bildfunk+++
Waandamanaji nchini Yemen wakisherehekea kuondoka kwa Rais Abdullah Ali SalehPicha: picture alliance/dpa

Alisema pia kwamba Rais Saleh alifanyiwa operesheni mbili zilizofaulu, moja ilikuwa kuondosha kipande cha marisawa ya kombora kutoka kifuani, na nyingine kutoka kwenye mshipa shingoni. Hatua itakayofuata itakuwa kufanyiwa operesheni ya kuziba majaraha kwa kutumia ngozi nyingine ya sehemu ya mwili wake. Msemaji huyo alisema kipindi cha kuuguliwa kitakuwa wiki mbili, na baada ya hapo atarejea Sanaa.

Afisa mwengine huko Yemen alisema Saleh alipata majeraha ya kuungua uso na kifuani, akisema alijeruhiwa kidogo nyuma ya kichwa chake; hivyo kujaribu kuwatuliza watu kwamba rais huyo hayuko mahututi. Mkasa huo ulimpata Saleh pale alipokuwa akisali msikitini ndani ya uwa wa jengo la rais. Lawama ya shambulio hilo ametwikwa kiongozi wa kikabili anayeipinga serikali, Sheikh Sadiq al-Ahmar, ambaye wapiganaji wake wamekuwa wakipigana na majeshi ya serikali.

Ofisi ya Sheikh Sadiq al-Ahmar imekubali kusitisha mapigano kwa masharti, na imekubali kuondosha majeshi yake kutoka majengo ya serekali baaad ya kuombwa na makamo wa rais, Abdrabuh Mansur Hadi.

Uamuzi wa Saleh kwenda kutibiwa Saudi Arabia, nchi muhimu katika eneo la Ghuba ya Uarabu, unaweza kurahisisha juhudi za kumtenga rais huyo kutoka madaraka baada ya kuiongoza nchi hiyo ilio maskini kabisa Arabuni kwa muda wa miaka 33.

Walimwengu wana wasiwasi zaidi juu ya mustakbali wa Yemen, kwa vile katika nchi hiyo wanaharakati wa mtandao wa kigaidi wa al-Qaida wana maficho yao.

Pia Ujerumani imefunga ubalozi wake mjini Sanaa, na taarifa ya wizara ya mambo ya kigeni mjini Berlin ilisema kwamba wafanya kazi waliobakia wa ubalozi huo wataondoka Yemen kwa haraka kama iwezekanavyo. Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Guido Westewelle, alisema:

Guido Westerwelle und Angela Merkel Rede im Bundestag Afghanistan Regierungserklärung
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle.Picha: AP

"Dola zenye kusambaratika ,dola zilizo katika vita vya kienyeji-kama ilivyo sasa Yemen- ni za hatari sana, zina hatari kwa vile kuna maeneo ambako ugaidi wa kimataifa unatafuta hifadhi zilizo za usalama kwao, na kutoka huko kufanya harakati zao."

Mwandishi: Miraji Othman/afp/Reuters

Mhariri. Mohamed Abdulrahman