1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Musharraf leo kung´atuka ukuu wa majeshi

27 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CTiC

ISLAMABAD.Rais Pervez Musharraf wa Pakistan leo hii anatarajiwa kung´atuka katika cheo cha ukuu wa majeshi, ikiwa ni siku moja kabla ya kuapishwa kuwa rais hapo kesho.

Taarifa hiyo ya General Musharraf imekuja huku kukiwa na hali ya hatari aliyoitangaza.

General Musharraf amekuwa katika mbinyo mkubwa ndani na nje kumtaka kuachia wafidha huo wa ukuu wa majeshi.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo Nawaz Sharif aliyerejea juzi kutoka uhamishoni, amesema kuwa kuingia kwake katika kinyang´anyiro cha uchaguzi mkuu hapo tarehe 8 January mwakani kutategemea na kuondolewa kwa hali ya hatari iliyowekwa na General Musharraf.