1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Musharraf bado ataka kugawana madaraka

2 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBTR

ISLAMABAD:

Serikali ya Pakistan imearifu kwamba ingali ina hamu ya kugawana madaraka na waziri mkuu wa zamani Benaizir Bhutto-waziri wa serikali ya jamadari Musharraf,amesema hii leo.Taarifa hiyo imetoka siku moja baada ya kiongozi huyo wa Upinzani Benazir Bhutto kuarifu mazungumzo ya miezi kadhaa na serikali ya Musharraf yamekwama.Akanadai kwamba anapanga kurejea nyumbani Pakistan kutoka Uhamishoni mjini London na kutoa tangazo la lini kufanya hivyo baada ya wiki 2.

Bibi Bhutto akielezea shabaha zake tatu anazolenga nchini Pakistan alisema.

„Tunapigania kuwa na mustakbal wa siasa za wastani kwa Pakistan;tunapigania mustakbal wa demokrasia kwa Pakistan na tunapigania Pakistan ambayo emeepukana na vitendo vya kigaidi ili iwezekane kutekeleza mahitaji ya umma yale ya kijamii hata ya kiuchumi.“wetu tangu