1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mursi kuapishwa leo

Abdu Said Mtullya30 Juni 2012

Rais mteule wa Misri Muhammed Mursi ameazimia kupambana kwa niaba ya watu wake na amewaonyesha majenerali upinzani kwa kusoma kiapo cha ishara cha kuingia madarakani mahala ambapo mapinduzi yalianzia.

https://p.dw.com/p/15OVQ

Muhammed Mursi ambae ni Rais wa kwanza mwenye msimamo wa kiislamu pia ametoa ahadi inayotarajiwa kuufanya uhusiano baina ya Misri na Marekani uwe mgumu. Mursi ameazimia kufanya juhudi ili Sheikh Omar Abdel-Rahman afunguliwe. Sheikh Abdul-Rahman asieona anatumikia kifungo cha maisha jela nchini Marekani kwa kosa la kula njama za kuripua sehemu muhimu katika mji wa New York na kwa kula njama za kutaka kumuua aliekuwa Rais wa Misri Hosni Mubarak.

Mursi pia ameahidi kuwa atawaachia wapinzani wote waliowekwa mahabusi ambao wamo hatarini kufikishwa mbele ya mahakama za kijeshi.Mursi ameahidi kufanya kila juhudi ili wafungwa wote waachiwe ikiwa pamoja na Sheikh Abdel-Rahman, kiongozi wa kidini wa watu waliotiwa hatiani mnamo mwaka 1993 kwa shambulio la bomu katika makao ya "World Trade Centre" Huku akishangiliwa na maalfu ya watu kwenye uwanja wa Tahrir Rais mteule wa Misri aliwaambiwa watu wake kwamba hakuna atakaeyachukua mamlaka yake. Amesema hakuna mamlaka yatakayokuwa juu ya "mamlaka haya" Licha ya kauli kali Muhammed

Egypt's Islamist President-elect Mohamed Mursi waves to people while surrounded by his members of the presidential guard in Cairo's Tahrir Square, June 29, 2012. Mursi took an informal oath of office on Friday before tens of thousands of supporters in Cairo's Tahrir Square, in a slap at the generals trying to limit his power. REUTERS/Amr Abdallah Dalsh (EGYPT - Tags: POLITICS CIVIL UNREST)
Mursi akiwa uwanja wa TahrirPicha: Reuters

Mursi aliepuka mvutano wa ana kwa ana na viongozi wa jeshi. Anatarajiwa kuapishwa rasmi leo kwenye sherehe zitakazofanyika kwenye mahakama kuu ya Misri.

Mwandishi: Abdul Mtullya/APE

Mhariri: Sudi Mnette