1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Munich 1860

Ramadhan Ali13 Juni 2007

Munich 1860 ndio ilivuma sana kabla hata Bayern Munich.Lakini leo imeangukia daraja ya pili ya Bundesliga.Miaka ya 1960 ndipo klabu hii ya pili ya jiji la Munich ilipotamba.

https://p.dw.com/p/CHbz

Je mimi ni Radi au mimi ni mfalme ? Hivyo ndivyo sahani za santuri zikihanikiza miaka ya 1960 na hasa mjini munich-kabla hata Bayern Munich kuanza kutamba.Radi hilo ni jina la mkato la Peter Radenkovic ,kipa maarufu alietamba enzi zile wa Munich 1860.Alikuwa maarufu sio kwa sauti yake tu bali hasa kwa mchezo wake wa ajabu hata enzi zile.

Kipa Radenkovic alikua na staili ya mchezo ya kulinda lango lake ambayo haikuwa tu ya kuvutia bali pia ya mafanikio.Miaka ya 1960ini ilikuwa miaka ya ushindi mkubwa katika historia ya Munich 1860.Simba kama klabu hii inavyojulikana ilinguruma kwa samba wake langoni-Peter Radenkovic aliejiunga na timu huyo kutoka kwao Yugoslavia.

Binafsi anakumbusha:

“Nikitupa macho nyuma wakati ule,basi naweza kusema kipindi cha mwaka 1963 hadi 1967,Munich 1860 ndio timu iliotamba sana katika historia ya Bundesliga nchini Ujerumani.Tulitawazwa mabingwa wa Ujerumani,tuliibuka makamo-bingwa,tulishinda kombe la shirikisho la dimba la Ujerumani na tulifika hata finali ya kombe la washindi barani Ulaya ingawa tulishindwa na West ham United yaUingereza.”

Anakumbusha kipa Radi.

“Wachezaji 3 wamejenga ukuta karibu na lango la wajerumani-nao ni Küppers,Wehner na Lutrop.Hurst aukiuka mpira na ukamfikia Moore.Waingereza wakashangiria bao.Ni mabao.2:0.”

Kwa mabao 2:0 Munich 1860 ililazwa na West Ham,United uwanjani Wembley.Tangu finali hiyo, Munich 1860-klabu tofauti kabisa na Bayern Munich-ilikaribia kuvaa taji la Ulaya.

Mchezo wao maridadi na wa kuonana wa miaka ya 1960ini ukaguatiwa na kuteremshwa klabu hii daraja ya pili miaka ya 1970ini.Hadi 1977,samba wa munich walishindwa kunguruma kurejea daraja ya kwanza ya Bundesliga.Baada ya hapo ikawa kuopanda ngazi na kushuka-msimu huu daraja ya kwanza na unaokuja wakirudi ya pili.

Mwishoe, 1982,Munich 1860 ikapokonywa leseni ya kucheza hata daraja ya pili na ikalazimishwa kuteremka daraja ya tatu.

Rudi Völler ambae wakati ule akiichezea Munich 1860,akaiacha mkono na kuhamia Werder Bremen ambako alikuja kutamba katika viwanja vya kimataifa.

Wakati munich 1860 ikikumbwa na misukosuko ule usemi: “ngoma ikivuma sana haikawii kupasuka” ukaisibu klabu hii.Mahasimu wao wa mtaani Bayern Munich -wakaanza kutamba,kwani samba hayupo nani tena wakutawala Munich isipokua Bayern ?

Wafadhili na vyombo vya habari vikahamia upande wa Bayern munich na enzi mpya ya dimba jijini humo ikaanza na kuselelea hadi leo.Ilipofika Machi,2004 rais wa muda mrefu wa Munich 1860 Wildmoser na mwanawe wa kiume walitiwa nguvuni kwa muda.Walituhumiwa walihongwa kitita cha Euro milioni 2.8 kuhusu kujengwa kwa uwanja mpya wa mpira.siku chache baadae,rais huyo hakuweza tena kubakia madarakani.Mwanawe akamtua mzigo wa lawama baba yake na akahiyari yeye aende korokoroni.

Alipon’gatuka Bw.Wildmoser ,hali ya munich 1860 ikazidi kuwa mbaya na hasa kifedha.Na tangu enzi hizo hata kimchezo, Munich 1860 haikufufuka.2004 iliteremshwa tena daraja ya pili ambako imebakia hadi leo.

Iliosalia kwa Munich 1860 ni kukumbuka zama zake za kipa wake maarufu-Radenkovic: