1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MUMBAI: Adhabu ya kifo kwa mashambulizi ya 1993

18 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBhR

Mahakama nchini India imetoa adhabu ya kifo kwa watu 3 waliokutikana na hatia ya kuhusika na mlolongo wa mashambulizi ya bomu mjini Mumbai katika mwaka 1993.Hii ni mara ya kwanza kwa adhabu ya kifo kutolewa kwa mashambulizi yaliyoua watu 257.Zaidi ya watu 100 wamekutikana na makosa ya kuhusika na mashambulizi hayo.Hadi hivi sasa, watu 14 wamepewa adhabu ya kifungo cha maisha. Inaaminiwa kuwa mashambulizi hayo ya bomu yalifanywa kulipiza kisasi kitendo cha wazalendo wa Kihindu cha kuubomoa msikiti katika mwaka 1992.