1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mtuhumiwa ahukumiwa kifungo.

18 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CdJp

Beirut.

Mtu mmoja anayeshutumiwa kuweka bomu katika sanduku katika treni nchini Ujerumani Jihad Hamad amehukumiwa kwenda jela miaka 12 na mahakama mjini Beirut.Mahakama hiyo imempata Hamad na hatia ya kuhusika katika njama za kuuwa watu katika treni nchini Ujerumani mwaka 2006. Mwenzake Yousef al-Haj Dib mwenye umri wa miaka 23 amehukumiwa kifo akiwa hayupo nchini humo na mahakama hiyo mjini Beirut. Raia huyo wa Lebanon mwenye umri wa miaka 22, Yousef el-Hajdib , anatuhumiwa kwa kujaribu kushambulia kwa mabomu treni ya abiria mjini Kolon mwaka jana.

Akitetea mteja wake wakili wa Yousef al-Haj Dib Johannes Bausch amesema.

Mabomu hayo yaliwekwa ndani ya treni lakini mabomu yote mawili yalishindwa kulipuka. Hajdib anashtakiwa kwa mauaji , na sio njama za ugaidi, kama sheria ya Ujerumani inavyosema wakati inahitajika watu watatu ndio iweze kuhesabiwa kuwa njama ya ugaidi.