1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mtu kujipima mwenyewe UKIMWI

8 Julai 2012

Marekani imetangaza kuwa inaruhusu kuuzwa kwa chombo cha kupima virusi vinavyosababisha UKIMWI kwa binaadamu vya HIV. Chombo hicho sawa na kijisanduku kidogo kitawasaidia Wamekani kujipima wenyewe HIV majumbani .

https://p.dw.com/p/15TO3
Sehemu za familia mbalimbali duniani
Sehemu za familia mbalimbali dunianiPicha: AP

Badala ya utaratibu wa sasa wa kwenda hospitalini na katika vituo maalumu vya Afya kutambua afya zao. Kiongozi wa Mamlaka ya Chakula na dawa wa taifa hilo (FDA) na Kampuni  iliyofanikisha kutengeza kikasha hicho ya  OraSure Technologies cha kupima  virusi vya HIV1 na HIV2, kwa pamoja wanasema hatua za tekinolojia hiyo ni  kubwa katika kupambana na maambukizi ya UKIMWI.

Alama ya kuonyesha kujali na kujikinga na UKIMWI
Alama ya kuonyesha kujali na kujikinga na UKIMWIPicha: picture-alliance/dpa

Ute na mate kuchukuliwa kutoka mdomoni

Wamesema anachotakiwa mtu kufanya ni kuchukuwa ute au mate yaliyopo katika kinywa chake kwa kutumia vifaa maalumu na kusugua katika fizi za juu na chini  kisha kuweka ute huo katika kipimo ambapo baada ya dakika kati 20 na 40 jawabu hupatikana

Kifaa hicho kinatarajiwa kupatikana  kwa matumizi mwezi oktoba mwaka huu kwa wauzaji wa maduka ya rejareja zaidi ya 30,000 watakaokuwa na uwezo wa kuuza kifaa hicho ambacho kinaweza kuwa msaada wa  kupunguza kufunga safari  kwenda   vituo vya afya kupima.

Mamlaka ya chakula na madawa ya  taifa hilo imesema ni kweli kifaa hicho  kinauwezo wa kupima ukimwi lakini   katika watu 12 watakaopima mtu mmoja kuna dalili ya kuwa na majibu chanya wakati hana virusi vya ugonjwa huo ambao ni miongoni mwa magonjwa yanayosababisha vifo vya watu wengi duniani.

Ufanisi wa kipimo hicho

Lakini ufanisi wake ni kwa asilimia 92  wakati asilimia 8 inayobakia ndipo  anaweza kupatikana mtu mmoja kuwa na majibu chanya wakati majibu yake  ni hasi. Huwezo wa kifaa hicho unawekwa wazi kuwa unaweza kutambua aina mbili za virusi vya UKIMWI yaani HIV namba 1na HIV namba 2 ambavyo hapo awali ilikuwa vigumu kuweza kutambua kwa kipimo kimoja.

Hali ya kwenda kwa wataalamu wa Afya kupata uhakika wa kupima haiepukiki kwani katika kila anayepima anashauriwa kuwaona wataalamu hao kuhakikisha suala hilo kwani  si  uhakikia wa asilimia100.

Maoni juu ya utafiti mwingine

Kulingana na utafiti mwingine uliofanya  juu ya huwezo wa kipimo hicho unasema wazi kuwa kati watu 5000  wanaopima ni mtu mmoja tu anatapa  majibu yasiyo sahihi kwa ungowa huo, ambapo Mamlaka ya Chakula na Dawa  ya Taifa hilo wanasema wanakubaliana  nalo.

Mtu akiwa ameshika kopo lenye vidonge vya kuongeza maisha kwa wagonjwa wa UKIMWI
Mtu akiwa ameshika kopo lenye vidonge vya kuongeza maisha kwa wagonjwa wa UKIMWIPicha: AP

Naye msemaji wa kampuni hii ya  OraSure Technologies anasema bei ya  kifaa hicho ni sawa na Euro 17 ambayo sawa na shilingi 3400 za Kenya na sawa na shilingi 34000 za Tanzania.

Wakati huo huo Rais na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hii Douglas Michels  anasema kifaa chao kitawasadia mno  watu kupima na kutambua hali  ya maambukizi ya UKIMWi kwa amani wakiwa nyumbani na wataklwenda kuwaona madaktari pale watakapo takiwa kufanya hivyo kwa matibabu zaidi.

Kulingana na kituo cha Kupambana na Kujikinga na Mangojwa cha Marekani mpaka sasa nchi hiyo ina watu milioni1.2 wanaoishi na virusi  vya HIV ambapo katika kila Wamerekani watano mmoja hatambui uzima wahali yake ya  afya  kama ana virusi hivi au la,huku kila mwaka  watu 50,000 wanaambukizwa virusi vinayosababisha UKIMWI.

Mwandishi:Adeladius Makwega/AFPE.

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman