1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Msomali aapishwa kuwa mbunge Marekani

Sekione Kitojo
4 Januari 2017

Ilhan Omar wa chama cha Democrat anakuwa Mmarekani wa kwanza mwenye asili ya Somalia kuapishwa kuwa mbunge akiliwalikisha jimbo la Minnesota linalokaliwa na Wasomali wengi zaidi Marekani.

https://p.dw.com/p/2VEev
Ilhan Omar
Picha: Getty Images/S. Maturen

Mbunge huyo mwenye umri  wa miaka 34 alianza rasmi kazi yake hiyo jana (Januari 3) mjini Saint Paul.

Ilhan alichaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka jimbo la Minnesota katika uchaguzi wa Novemba 8, ambao pia ulimuingiza madarakani Donald Trump kuwa rais wa Marekani, huku akiendesha kampeni ya kupinga wageni, na hasa Waislamu. 

Mwanamke huyo aliyewahi kuishi kwenye kambi ya wakimbizi nchini Kenya, aliwasili Marekani mwaka 1995, akiwa mtoto pamoja na familia yake wakikimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Somalia.  

Alianza kuvutiwa na masuala ya siasa akiwa na umri wa miaka 14. Katika jimbo la Minnesota, kunaishi watu 40,000 wenye asili ya Somalia, ikiwa ni idadi kubwa kuliko jimbo jengine lolote nchini  Marekani.