1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Msichana alohukumiwa kifo kwa kuua apunguziwa adhabu

Lilian Mtono
27 Juni 2018

Msichana Noura Hussein mwenye umri wa miaka 19 aliyehukumiwa kifo kwa kosa la kumuuwa mumewe sasa atatumikia kifungo cha miaka mitano

https://p.dw.com/p/30NWL
Facebook-Kampage Justice for Noura
Picha: facebook.com - Justice for Noura

Msichana aliyehukumiwa kifo kwa madai ya kumuua mume wake nchini Sudan, ambaye alidai alimbaka amepunguziwa adhabu hiyo hadi kifungo cha miaka mitano jela, baada ya rufaa.

Kulingana na wakili wake, Abdullah Ibrahim aliyezungumza na shirika la habari la dpa, mahakama ya mjini Khartoum ilipunguza adhabu hiyo dhidi ya msichana huyo Noura Hussein pamoja na kumtaka kulipa fedha ya damu kwa familia ya mumewe.

Kulingana na wanaharakati wanaopinga adhabu ya kifo, shirika la Amnesty International, Noura alilazimishwa kuolewa akiwa na miaka 16, na baada ya kuolewa alibakwa na mumewe, wakati akiwa ameshikiliwa na ndugu zake watatu wa kiume, na alipojaribu kumbaka tena ndipo inapodaiwa alimchoma kisu ili kujilinda.