1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mshindi wa zawadi ya Nobel Herta Müller

8 Oktoba 2009

Uandishi-sanifu kwa mrumania wa asili ya kijerumani.

https://p.dw.com/p/K2LV
Bibi Herta Müller-mshindi wa zawadi ya Nobel.Picha: AP

Zawadi ya Nobel kwa uandishi-sanifu mwaka huu,ametunukiwa Mrumania wa asili ya Ujerumani: Bibi Herta Müller.Utotoni na ujana wake, aliupitisha chini ya utawala wa kitisho wa Rumania na akahadithia hali hiyo katika vitabu vyake.Tangu mwanzoni mwa miaka ya 1990, na baada ya kutafsiriwa vitabu vyake katika lugha zaidi ya 20,Herta Müller,amekuwa mmoja wa waandishi maarufu wa fani ya uandishi sanifu ulimwenguni.1987,Bibi Herta Müller na mumewe, waliomba ruhusa kuondoka Rumania kuhamia Ujerumani.

Pale Katibu wa Taasisi ya Sweden ya zawadi ya Nobel, Peter Englund, alipotangaza mshindi wa zawadi hiyo kwa mwaka huu wa 2009,kulikuwapo na shangwe ukumbini.

Kwamba imesadifu mara hii ametunzwa Bibi Herta Müller, haikumsangaza mtu.Mara tu baada ya kujulikana ni yeye, mtu mmoja alikamata nakala ya gazeti la Stockholm (EXPRESSEN) mbele ya kamera likiwa na kichwa cha habari: "Mshindi wa zawadi ya Nobel kwa uandishi sanifu ni Herta Müller".

Kwani, waandishi vitabu wengi wa Kiswede na idara za uandishi wa kitamaduni,wakimpigia debe mnamo miaka iliopita, Bibi Herta Müller.Miongoni mwao hata mkosoaji uandishi-sanifu Ulkrike Milles:

"Ni muandishi bora kabisa wa vitabu niliewahi kusoma .Ni mwenye ustadi kabisa wa uandishi fasihi.Isitoshe, ni mtu anaeheshimika.Uchambuzi wake ni mkali kama kisu,huandika kwa uwazi na huyapima barabara maneno yake anayoandika na ni mcheshi sana."

Bibi Herta Müller, alizaliwa 1953 huko Nitzkydorf,kijiji kidogo cha Jamii ya warumania wa asili ya Ujerumani.Akasomea fani ya lugha ya kijerumani-germanistik- na uandishi wa kirumania,lakini hakuruhusiwa kuchapisha vitabu vyake nchini Rumania. Sababu ni kuwa akikataa kuifanyia kazi Idara ya Usalama ya rumania (Securitate). 1987, pamoja na mumewe, waliweza kuhamia Ujerumani.Ukosefu wa nchi yako ulikozaliwa kukageuka mada kuu ya maandishi yake.

"Sikuwahi kuandika kwa lugha ya kirumania.Ingawa nimekulia na lugha hiyo na naweza kuiandika.Licha ya kuwa lugha ya kijerumani ndio nikiandikia,hufikiri kirumania."

Katika riwaya yake ya karibuni alioita "Atemschaukel" ambayo imeteuliwa kupendekezwa kwa zawadi ya vitabu ya Ujerumani Jumatatu ijayo, alielezea jinsi kiajana mmoja katika kambi ya wafungwa ya waliosafirishwa Russia. Yaliomo ndani ya kitabu hicho, ni mfano halisi wa hatima ya warumania wa asili ya kijerumani 80.000 baada ya vita vya pili vya dunia.Kwanini hali hutokea hivyo ? -anajiuliza muandishi Herta Müller .

"Kwanini daima katika ulimwengu huu kuna watu wanabidi kuzikimbia nchi zao ili kuokoa maisha yao na wengine hufanya madhambi ya uhalifu,wakaivuruga nchi na kuifanya kana kwamba ni mali yao ?

Idara ya Usalama ya Rumania "Securitate", ilijaribu baada ya bibi Müller kuhamia Ujerumani kumvunjia hadhi na jina lake kuwa eti kila mara, akiviandikia vyombo vya habari vya kijerumani na eti alikuwa jasusi.

Baada ya kumalizika vita baridi,Bibi Herta Müller, ambae tangu 1995 ni mwanachama wa Taasisi ya Ujerumani ya lugha na utungaji mashairi,akiweza kuitembelea nchi yake alikozaliwa:Rumania,maskani ambayo lakini imegeuka nchi ya kigeni kwake.

Mwandishi:Breitschuh, Albrecht/ARD/ZDF/ Ramadhan Ali

Mhariri:Abdul-Rahman