1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mpiga kura kutojitokeza licha ya kufuatwa kwa helikopta

Yusra Buwayhid
9 Agosti 2017

Licha ya IEBC kupeleka maafisa wake kwa helicopta kumfuata mpiga kura pekee katika kituo cha LochorApua, Loitamoe Eripon, alishindwa kujitokeza kupiga kura yake.

https://p.dw.com/p/2hw5j
Der Hubschrauber MI 17
Picha: picture alliance/dpa/K. Rostislav

Mpigaji kura nchini Kenya, Loitamoe Eripon, ambaye alikuwa ni mtu pekee aliyejiandikisha kupiga kura katika kituo cha LochorApua, Jimbo la Turkana Magharibi, hakujitokeza kutimiza haki yake ya kikatiba, Jumanne siku ya uchaguzi mkuu. Maafisa wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Kenya IEBC ambao walitembelea kituo hicho kwa kutumia usafiri wa helikopta ili kuhakikisha Eripon anatimiza haki yake ya kikatiba ilibidi warudi walipotoka kwa sababu bwana huyo hakujitokeza kupiga kura kituoni. Jimbo la Turkana Magharibi linapakana na nchi jirani ya Sudan Kusini.

Mwandishi: Yusra Buwayhid

Mhariri:Iddi Ssessanga