1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSUL : Watu 45 wauwawa nchini Iraq katika miripuko

6 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBbX

Nchini Iraq takriban watu 45 wameuwawa katika shambulio la kujitolea muhanga maisha katika kijiji cha Al Quba na mjini Baghdad leo hii.

Shambulio katika kitongoji cha Washia limetokea wakati lori lilosheheni mabomu liliporipuliwa na kuuwa watu 30 na kujeruhi wengine kadhaa na kuteketeza nyumba 20 ambapo 10 kati yao zikiwa zimeteketezwa kabisa.

Mashambulio katika maeneo mengine yameuwa watu wengine 15 ikiwa ni pamoja na watu tisa waliouwawa mjini Baghdad wakati bomu lililotegwa barabarani kuripuka kwenye kituo cha mabasi kisicho rasmi ambayo hutumiwa na maelfu ya watu mjini Baghdad.