1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOSCOW:waziri mkuu mpya aidhinishwa na bunge

Bunge la Urusi limemuidhinisha bwana Viktor Zubkov kuwa waziri mkuu mpya wa nchi hiyo siku mbili baada ya rais Vladimir Puttin kumteuwa.

Bwana Zubkov ambae anaonekana kuwa mtiifu kwa rais Puttin amehakikisha kwamba ataendeleza sera za rais Vladimir Puttin ili kudhibiti utulivu na mafanikio zaidi ya uchumi wa Urusi.

Waziri mkuu huyo mpya amedokeza kuwa mawaziri wasio wajibika watafukuzwa kazi.

Waziri mkuu mpya wa Urusi Viktor Zubkov amechukuwa nafasi ya waziri mkuu wa zamani Mikhail Fradkov aliyetimuliwa na rais Puttin.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com