1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOSCOW:Urusi yakemea mpango wa makombora ya ulinzi ulaya mashariki

Waziri wa mambo ya nje wa Urussi Sergei Lavrov ameitaka Marekani kusimamisha mazungumzo yake kuhusu makombora ya ulinzi na jamhuri ya Czech na Poland hadi watakapojadiliana juu ya suala hilo.

Matamshi hayo yamekuja siku moja baada ya rais Bush kukutana na mwenzake wa Poland Lech Kachinski na kuashiria kuendelea na mpango huo wa kuweka makombora ya ulinzi ulaya mashariki.

Mpango huo wa Marekani umezusha mvutano mkubwa kati ya serikali ya mjini Washington na Moscow katika kipindi cha miezi kadhaa sasa.

Wakati huo huo rais Vladmir Putin amelikosoa shirika la biashara duniani WTO akisema ni chombo kisichozingatia demokrasia,kilichopitwa na wakati na kisochokuwa na ustadi. Akizungumza katika jukwaa la kiuchumi leo hii rais Putin amesema paundwe shirika jingine mbadala ambalo litazingatia uchumi wa nchi zinazoendelea.

Matamshi ya Putin yanatokea wakati ambapo waziri wa ngazi ya juu wa Urussi amefanya mazungumzo na wajumbe wa Ulaya na Marekani kuhusu juhudi za Urussi za kutaka kujiunga na shirika hilo la WTO

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com