1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW:Putin atisha kulipiza kisasi makombora ya kujihami

4 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBuu

Rais wa Urusi Vladimir Putin anaionya Marekani kuwa kuweka makombora ya kujihami katika eneo la Ulaya Mashariki huenda kukasababisha wao kurusha makombora ya kulipiza kisasi.

Urusi inatilia shaka mipango ya Marekani ya kuweka makombora ya kujihami katika Ulaya mashariki kwa kuhofia kushambuliwa na makombora ya Iran au taifa jengine lililo na uwezo.

Kulingana na Rais Putin nchi ya Iran haina uwezo wa kufany hilo.Kwa upande wake lengo hasa la Marekani ni kuichokoza Urusi ili kulipiza kisasi kwa madhumuni ya kuvunja uhusiano kati ya Urusi na Ulaya.

Marekani inapanga kuweka makombora hayo ya kujihami nchini Poland.