1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW:Iran kuwekewa vikwazo vikali zaidi

21 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCGo

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linapanga kupiga kura wiki hii itakayoidhinisha Iran kuwekewa vikwazo vipya baada ya kukataa kusitisha mpango wake wa kurutubisha madini ya uranium.Kulingana na Marekani mpango huo huenda ukatumika kutengeza silaha za nuklia jambo inalokanusha nchi ya Iran.

Kwa upande mwingine nchi ya Urusi inasema kuwa haiungi mkono hatua ya kuiwekea Iran vikwazo vikali zaidi kwa mujibu wa Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov.

Urusi iliyo na ushirikiano wa kisiasa na kibiashara nchini Iran ina kura ya turufu katika Baraza la Usalama jambo linaloipa uwezo wa kumaliza nguvu mapendekezo ya kuiwekea Iran vikwazo vikali.Urusi inashikilia kuwa wanakubaliana na mtizamo wa mataifa y magharibi ila wanaamini kuwa majadiliano na kufikiwa muafaka ni muhimu zaidi.

Mataifa ya Afrika Kusini na Indonesia yanapendekeza kufanyiwa mabadiliko kwa azimio la Umoja wa mataifa kuhusu mkataba wa kuzuia ueneaji wa silaha za nuklia.Urusi inaunga mkono hoja hiyo.

Afrika Kusini inatoa wito kwa kusimamishwa kwa vikwazo vyote dhidi ya Iran na mazungumzo kuanzishwa upya.

Iran kwa upande wake inashikilia kuwa ina haki ya kuwa mpango wa nuklia wa kutengeza nishati na kukanusha kuwa inapanga kutengeza silaha za nuklia.