1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW:Bush akubaliana na Putin juu ya mpango wake wa kuweka makomboraya kujihami Ulaya

29 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCEb

Rais George Bush wa Marekani amemwambia Rais Vladmir Putin wa Urusi kuwa anajiandaa kufanya naye majadiliano ya kina juu ya mpango wa Marekani kuweka makombora ya kujihami Ulaya.

Katika taarifa yake Ikulu ya Urusi Kremlin, imesema kuwa viongozi hao walifanya mazungumzo ya simu juu ya suala hilo.

Jamuhuri ya Czech, imetangaza kuwa inaingia katika majadiliano rasmi na Marekani juu mipango ya nchi hiyo kutaka kuweka sehemu ya makombora yake ya kujihami katika ardhi yake

Marekani inataka kuweka makombora ya kujihami na kile inachosema mashambulizi ya nchi kama Iran na Korea Kaskazini.

Mapema Ujerumani ambayo kwa sasa ni rais wa Umoja Ulaya iliitaka Marekani kufanya mazungumzo na Urusi juu ya mpango wake huo, kabla ya kuutekeleza.