1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW : Yeltsin azikwa kwa heshima za taifa

26 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC73

Rais wa kwanza wa Urusi aliechaguliwa kidemokrasia Boris Yeltsin amezikwa kwenye makaburi ya Moscow hapo jana kufuatia maziko ya heshima zote za taifa katika Kanisa la Kiorthodox la Yesu Muokozi.

Maziko yake yamehudhuriwa na Rais wa sasa wa Urusi Vladimir Putin, waheshimiwa mbali mbali wa kigeni pamoja na marais wa zamani wa Marekani Bill Clinton na George Bush. Ujerumani iliwakilishwa na Rais Horst Köhler.

Yeltsin aliefariki hapo Jumatatu kutokana na mshtuko wa moyo alikuwa rais wa Urusi kuanzia mwaka 1991 hadi alipojiuzulu mwaka 1999.

Anapongezwa kwa kuiweka Urusi kwenye njia ya demokrasia na uchumi unaotegemea nguvu za soko lakini kipindi chake madarakani pia kimeshuhudia kuzorota kwa uchumi na vita vya kwanza dhidi ya waasi wa Chechnya wanaotaka kujitenga .