MOSCOW: Waziri Mkuu wa Urusi amejiuzulu | Habari za Ulimwengu | DW | 12.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOSCOW: Waziri Mkuu wa Urusi amejiuzulu

Rais Vladimir Putin wa Urusi ameivunja serikali ya Waziri Mkuu Mikhail Fradkov.Putin amechukua hatua hiyo kuambatana na ombi la Fradkov.Miongoni mwa sababu zilizotolewa na Fradkov ni matukio muhimu ya kisiasa yanayotazamiwa nchini humo katika miezi ijayo.Vile vile anataka kumuachia Putin uhuru kamili wa kujiamulia katika uteuzi wa mawaziri.Rais Putin amempendekeza mtaalamu wa fedha,Viktor Subkov kushika wadhifa wa waziri mkuu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com