MOSCOW: Urusi yawarejesha nyumbani raia wa Georgia | Habari za Ulimwengu | DW | 06.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOSCOW: Urusi yawarejesha nyumbani raia wa Georgia

Urusi imewarejesha nyumbani raia wa Georgia waliotuhumiwa kuwa wahamiajai wasio halali. Raia hao walikamatwa wakati wa msako wa polisi ulioendelea katika siku chache zilizopita.

Hatua hiyo ni mojawapo ya juhudi za Urusi kukatiza uhusiano na Georgia, huku mgogoro wa kidiplomasia baina ya nchi hizo mbili ukizidi.

Raia hao walipelekwa katika uwanja wa ndege wa kijeshi nje ya mji wa Moscow na kutiwa katika ndege kurudishwa kwao. Msemaji wa wizara ya mashauri ya kigeni wa Georgia amesema ndege inayowabeba raia hao inatarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa Tbilisi katika saa chache zijazo.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Urusi, Sergei Lavrov, anasema Urusi haina makosa ila yenye makosa ni Georgia.

´Nina maana kwamba utawala wa Georgia lazima uchukue hatua. Serikali inafahu vizuri kabisa matatizo yalipo. Tunatarajia imalize sera zake za kuipinga Urusi. Ni njia hiyo pekee itakayomaliza matatizo yaliyopo kwa sasa.´

Wakati huo huo, mwenyeti wa shirika la usalama la kimataifa barani Ulaya, OSCE, ameitolea mwito Urusi irudishe uhusiano wake na taifa jirani la Georgia.

Akizungumza mjini Brussels waziri wa mashauri ya kigeni wa Ubelgiji, Karel De Gucht, amezitaka Georgia na Urusi zimalize mzozo wao wa kisiasa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com