1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Urusi yafanya jaribio la kombora jipya

30 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBwc

Urusi imesema imefanya jaribio la kombora jipya lililo na vichwa kadhaa na linaloweza kupasua aina yoyote ya mfumo wa ulinzi duniani, ikiwa ni pamoja na mfumo wa ulinzi wa Marekani unaopangwa kuwekwa mashariki mwa Ulaya.

Jeshi la Urusi limesema kombora aina ya RS – 24 lilivurumishwa kutoka kambi ya jeshi iliyo kaskazini mwa mji mkuu Moscow na saa moja baadaye likapiga mahali lilipotakiwa kulenga katika eneo la Kamchatka kwenye bahari ya Pacific umbali wa kilomita 6,000.

Utawala wa rais George W Bush umesema mpango wake wa usalama, ambao sehemu itawekwa nchini Poland na jamhuri ya Cheki, hautailenga Urusi bali nchi kama vile Iran.

Akizungumza na waziri mkuu wa Ureno, Jose Socrates, ambaye atachukua urais wa Umoja wa Ulaya Julai mosi mwaka huu, rais wa Urusi, Vladamir Putin, alionya kwamba mpango wa usalama wa Marekani utaibadili Ulaya kuwa utambi unaoweza kulipuka wakati wowote.