1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Rice akutana na wahariri na mtoto wa mkosoaji wa serikali Politkovskaya

22 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD0G

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani,Condoleezza Rice wakati wa ziara yake mjini Moscow,amekutana na wahariri na mtoto wa kiume wa muandishi wa habari wa Kirussi Anna Politkovskaya alieuawa. Politkovskaya aliekuwa mkosoaji wa serikali ya Moscow,aliuawa juma lililopita karibu na fleti yake.Wizara ya kigeni ya Marekani imesema,mkutano huo ni ishara ya kuunga mkono uhuru wa vyombo vya habari.Rais Vladimir Putin wa Urussi anatuhumiwa na makundi yanayotetea haki za binadamu na madola ya magharibi kuwa anapuza uhuru wa vyombo vya habari.Waziri Rice amekwenda Urussi baada ya kuzitembelea Japan,Korea ya Kusini na China. Wakati wa ziara yake barani Asia,Rice alitoa wito kwa nchi hizo kutekeleza kikamilifu vikwazo vilivyowekwa na Umoja wa Mataifa dhidi ya Korea ya Kaskazini baada ya nchi hiyo kufanya jaribio lake la kwanza la kinuklia mapema mwezi huu. Waziri wa kigeni wa Urussi,Sergei Lavrov anapinga hatua kali kuchukuliwa dhidi ya Korea ya Kaskazini na Iran.Amesema,itafutwe njia ya kurejea kwenye meza ya majadiliano kuhusu migogoro ya kinuklia ya nchi hizo mbili.