1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Rais Putini akutana na wazuiri mkuu wa Israel Ehud Olmert

18 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD1Y

Rais wa Urusi Vladamiri Putin amefanya mazungumzo na waziri mkuu wa Israel, Ehud Olmert mjini Mosccow hii leo. Mazungumzo hayo yametuwama hjuu ya juhudi za kutafuta amani ya Mashariki ya Kati na mipango ya nyuklia wa Iran na Korea Kaskazini.

Israel inapinga madai ya Iran kwamba mpango wake wa nyuklia ni wa kutengeneza nishati na wala sio silaha. Ehud Olmert amemwambia rais Putin kwamba Urusi inatakiwa kusaidia kuutanzua mzozo huo.

Mada nyengine iliyojadiliwa ni hatua ya Urusi kusafirisha silaha kwa Iran na Syria. Israel tayari imelalamika kwamba silaha zilizotengezwa nchini Urusi zilitumiwa na wanamgambo wa Hezbollah wakati wa vita vya kusini mwa Lebanon, walizozipata pengine kutoka Iran na Syria.