1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Rais Putin asema Marekani iweke muda wa kuondoa jeshi lake kutoka nchini Irak

18 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Ek

Rais Vladimir Putin wa Urusi amesema kuwa Marekani inastahili kuweka muda wa kuwaondoa wanajeshi wake kutoka nchini Irak.

Putin ameyasema hayo wakati wa mahojiano ya moja kwa moja katika televisheni juu ya maswala ya ndani na nje ya Urusi.

Rais Puttin amesema kadri Marekani inavyozidi kuchelewa kutangaza muda wa kuondoa vikosi vyake kutoka Irak utawala nchini humo nao unazidi kulegeza jitihada za kuunda vikosi vya kulinda usalama wa nchi yao.