1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moscow. Putin kuchukuwa wadhifa wa waziri mkuu .

2 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/CBKv

Katika hatua ya kushangaza , rais Vladimir Putin amesema anapanga kuchukuwa wadhifa wa waziri mkuu kwa kugombea kupitia chama kikuu nchini Russia kama mgombea wake mkuu katika uchaguzi utakaofanyika mwezi Desemba .

Putin amekiambia chama chake cha Allied United Russia mjini Moscow kuwa atabadilisha wadhifa iwapo mrithi wa kiti chake cha urais atakuwa mtu makini March mwaka ujao.Wiki iliyopita , Putin alimteua Viktor Zubkov kuwa kaimu waziri mkuu, akiashiria kuwa Zubkov huenda akawa mgombea wa kiti cha urais. Wachunguzi wa mambo wanasema kuwa hatua hiyo itamuwezesha Putin kubaki na udhibiti hata baada ya muda wake wa urais kumalizika pamoja na kufikia muda karibu ya kustaafu.

Jana Jumatatu moja kati ya vyama vinavyounda muungano wa upinzani , unaoongozwa kwa pamoja na bingwa wa zamani wa mchezo wa Chess Garry Kasparov amejisajili katika ofisi kuu ya uchaguzi kugombea katika uchaguzi mkuu wa mwezi Desemba. Kura ya maoni inaonyesha kuwa chama cha rais Putin United Russia kikiwa na asilimia 55, kikifuatiwa na Wakomunist wakiwa na asilimia 18.