Moscow. Putin ayahakikishia mataifa ya Balkan kuhusu nishati. | Habari za Ulimwengu | DW | 25.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Moscow. Putin ayahakikishia mataifa ya Balkan kuhusu nishati.

Rais Vladimir Putin wa Russia ameyataka mataifa katika eneo la Balkan kuwa na imani na Russia kuwa ni msambazaji mwaminifu wa nishati.

Katika mkutano na viongozi wa mataifa manane katika mji mkuu wa Croatia Zagreb, Putin ameahidi kusaidia kujengwa kwa bomba jipya la gesi katika eneo la Balkan.

Alijaribu kutuliza hofu ya uwezekano wa kusitisha usambazaji huo kwa kuwakumbusha kuwa Russia haijavunja wajibu wake wa kimkataba.

Viongozi hao pia walijadiliana kuhusu hadhi ya baadaye ya jimbo la Serbia la Kosovo.

Rais wa Serbia Boris Tadic amesema kuwa Kosovo iliyo huru inaweza kuathiri eneo lote. Russia inakataa mpango wa umoja wa mataifa unaoungwa mkono na Marekani na mataifa ya umoja wa Ulaya ambao unataka kutoa uhuru kwa jimbo la Kosovo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com