MOSCOW: Polisi waanza kuchunguza stakabadhi za shule | Habari za Ulimwengu | DW | 06.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOSCOW: Polisi waanza kuchunguza stakabadhi za shule

Polisi wa Urusi wameanza kuchunguza stakabadhi za shule katika juhudi za kuwatafuta wahamiaji wasio halali raia wa Georgia, huku operesheni ya kukata mahusiano na Georgia ikiendelea.

Urusi pia imeamuru biashara zinazomilikiwa na Georgia nchini humo zichunguzwe. Mikahawa miwili na hoteli inayomilikiwa na raia wa Georgia zimevamiwa na maofisa wa usalama, zikilaumiwa kwa kukwepa kodi.

Wakati huo huo, idara ya uhamiaji ya Urusi imesema inarefusha muda wa kusimamisha utoaji wa visa za kusafiria kwa raia wa Georgia na visa za miezi sita zilizopewa raia wa Georgia zitapunguzwa hadi miezi mitatu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com