1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moscow. Mzozo wa Russia na Georgia wazidi kukua.

8 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD52

Russia imekataa ombi la shirika la usalama na ushirikiano barani Ulaya la kupatanisha katika juhudi za kumaliza mzozo unaozidi kukua baina ya serikali ya Russia na Georgia.

Maafisa wa Russia wamefunga biashara zinazoendeshwa na watu kutoka Georgia, na kuwarejesha nyumbani kiasi cha wahamiaji 150 wa Georgia na kuamuru kufanya msako dhidi ya wanafunzi raia wa Georgia wanaosoma mjini Moscow.

Polisi pia wamewakamata vijana kadha ambao wamekuwa wakifanya maandamano wakiunga mkono Georgia nje ya ubalozi wa Russia.

Mzozo huo ulizuka wiki iliyopita , wakati Georgia ilipowakamata maafisa wanne wa kijeshi wa Russia kwa madai ya ujasusi.

Licha ya kuchiwa kwao, Russia imeweka vikwazo vya usafiri na huduma za posta kati ya nchi hizo.