1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW : Mzozo wa mafuta watatuliwa

13 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCbA

Urusi na Belarus zimetia saini makubaliano rasmi yenye kutatuwa mzozo wa kupitisha mafuta ambao umetibuwa usambazaji kupitia bomba kuu kutoka Urusi kwenda Ulaya.

Vyombo vya habari vya Urusi vimemkariri Waziri Mkuu wa Urusi Mikhail Fradkov akisema kwamba umefikiwa uvumbuzi unowiana.Makubaliano hayo yanahusu fani mbali mbali za taratibu za biashara ya mafuta kati ya nchi hizo ambapo serikali ya Urusi ilisema huko nyuma kwamba zinatumiwa visivyo haki na Belarus.

Mzozo huo ulisababisha kufungwa kwa bomba kuu la Urusi la kusafirisha mafuta nje hapo Jumatatu na kudumu hadi Jumaatano na hiyo kutibuwa usambazaji wa mafuta kuelekea nchi za Umoja wa Ulaya na kuchafuwa sifa ya Urusi kama ni nchi inayoweza kuaminika kwa usambazaji wa nishati.