1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moscow. Condi awasili nchini Russia.

14 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC22

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice amewasili nchini Russia kwa mazungumzo yenye lengo la kuweka sawa uhusiano ambao umeathirika kutoka na tofauti za mataifa hayo mawili.

Rice anatarajiwa kukutana na maafisa kadha wa Russia , pamoja na rais wa nchi hiyo Vladimir Putin.

Hali ya wasi wasi imejitokeza kutokana na masuala ya NATO pamoja na upanuzi wa kijeshi wa marekani kuelekea katika maeneo ambayo hapo zamani yalikuwa yakitawaliwa na Urusi pamoja na mipango ya uwekaji wa ngao ya ulinzi dhidi ya makombora katika Ulaya ya mashariki.

Marekani na Poland zinatarajiwa kuanza rasmi kujadili uwekaji wa maroketi 10 ambayo yatapambana na maroketi kutoka sehemu yoyote ili kama sehemu ya ngao hiyo, ambayo Russia inapingana nayo.

Russia pia inatofautiana na mpango unaoungwa mkono na Marekani ambao hivi sasa uko mbele ya umoja wa mataifa wa kulipatia jimbo la Serbia la Kosovo uhuru.