1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Morocco wachaguwa bunge jipya

Sylvia Mwehozi
7 Oktoba 2016

Wamoroko wanachagua bunge jipya ikiwa ni miaka mitano baada ya serikali ya vyama vya Kiislamu kuchukua madaraka kufuatia  maandamano yaliyochochewa na vuguvugu la kudai demokrasia katika nchi za Kiarabu.

https://p.dw.com/p/2R0t6
Marokko Wahlkampagne Anhänger vom Premierminister Benkirane
Picha: picture-alliance/dpa/A. Senna

Chama cha Haki  na Maendeleo (PJD) kinachofuata siasa za Kiislamu kinapambana na wapinzani wa kiliberali, ambao wanadai chama hicho kinataka "kuurudisha nyuma Uislamu" katika jamii ya  Morocco.

Licha ya wananchi kuamua nani aingie bungeni, mamlaka kamili yanasalia mikononi mwa Mfalme Mohammed VI, ambaye ni kizazi za utawala wa kifalme uliodumu kwa miaka 350 sasa katika taifa hilo la kaskazini mwa Afrika.

Katiba mpya iliyopitishwa wakati wimbi la mageuzi likivuma kwenye mataifa ya Kiarabu na kuziangazusha baadhi ya tawala, ilihamisha baadhi ya madaraka ya mfalme kwa bunge.

Hatua hiyo ilisaidia kuinusuru Morocco kwenda njia ya majirani zake wa Tunisia, Misri na Libya.

Serikali ya Waziri Mkuu Abdelilah Benkirane wa PJD inajumuisha pia Wakomunisti, Waliberali na Wahafidhina.

Chama hicho kinapigania muhula wa pili ili kuendeleza mipango yake ya mageuzi ya uchumi na kijamii.