1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MONROVIA: Rais Hu wa China ziarani nchini Liberia

1 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCW9

Rais Hu Jintao wa China hii leo anaizuru Liberia.Hicho ni kituo cha pili cha ziara yake ya siku 12 barani Afrika.Hu aliianza ziara yake nchini Cameroon ambako aliahidi kuipatia nchi hiyo ya Afrika Magharibi,misaada na mikopo yenye thamani ya zaidi ya Euro milioni 40.Ziara ya rais Hu inasisitiza msimamo wa China wa kutaka kuwa na uhusiano imara wa kiuchumi na bara la Afrika, ambalo lina akiba kubwa ya malighafi na mafuta yanayohitajiwa na China kwa uchumi wake unaokuwa kwa kasi kubwa.Lakini sera za China kuelekea Afrika zimekosolewa kwa sababu ya uhusiano wake wa karibu na nchi kama Sudan na Zimbabwe.