1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU:Somalia bado kwatokota

7 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCvL

Vikosi vya wapiganaji wa mahakama za kiislamu nchini Somalia wamesema wamepambana na wanamgambo wanaungwa mkono na jeshi la Ethiopia katika eneo la Kaskazini mwa Somalia.

Muungano wa mahakama za kiislamu umefahamisha kwamba wapiganaji wake wamepambana na wanamgambo hao karibu na mpaka wa eneo la Puntland eneo ambalo linamafungamano ya karibu na Ethiopia na ambalo limepinga kuenea kwa mahakama hizo zinazodhibiti sehemu nyingi za kusini mwa Somalia.

Hata hivyo maofisa wa Puntland wamekanusha kutokea kwa mapigano yoyote wakisema wapiganaji wa mahaka hizo wanatafuta sababu ya kulishambulia eneo hilo.

Wakati huo huo maofisa wa Ethiopia kwa mara nyingine wamekanusha kwamba wanajeshi wake wako nchini Somalia.