MOGADISHU:Mogadishu yashambuliwa kwa kombora | Habari za Ulimwengu | DW | 22.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOGADISHU:Mogadishu yashambuliwa kwa kombora

Wanamgambo walio na msimamo mkali nchini Somalia wanatisha kushambulia majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa Afrika kwa mabomu ya kujitoa muhanga waliopangwa kuwasili nchini humo katika siku kadhaa zijazo.Uwanja wa ndege wa kimataifa mjini Mogadishu umeshambuliwa kwa makombora hii leo.Wapiganaji wasiojulikana wamewapiga risasi maafisa wawili wa serikali mjini Mogadishu.

Wakati huohuo kundi jipya la wapiganaji walio na msimamo mkali la Popular Resistance Movement in the Land of the Two Migrations limetisha kushambulia majeshi ya usalama yanayopangiwa kuwasili nchini humo katika siku kadhaa zijazo.

Nchi ya Uganda iliyoahidi kupeleka majeshi yake katika mpango huo inasema kuwa vitisho hivyo vipya havitaizuia kuitimiza.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com