1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU:Mkutano wa maridhiano wafanyika leo

15 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBik

Mkutano wa kuleta maridhiano nchini Somalia unatarajiwa kuanza leo mjini Mogadishu.

Mkutano huo ulioahirishwa mara tatu unahudhuriwa na wajumbe alfu moja na mia tatu wanaowakilisha pande mbalimbali. Wadadisi wanasema mkutano huo unaweza kuleta suluhu baina ya makundi muhimu ya nchi.

Wapiganaji wa kiislamu wametishia kuuvuruga mkutano huo.Lakini ulinzi mkali umewekwa mahala ambapo mkutano huo utafanyika.