MOGADISHU:Mapigano makali yazuka Mogadishu | Habari za Ulimwengu | DW | 09.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOGADISHU:Mapigano makali yazuka Mogadishu

Mapigano makali yalizuka hapo jana usiku kati ya wanamgambo wakisomali na wanajeshi wa serikali ya mpito katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu.

Walioshuhudia mapambano hayo wanasema wanamgambo walifyetua roketi dhidi ya wanajeshi karibu na hospitali moja na kituo cha watoto yatima kaskazini mwa mji wa Mogadishu.Mapigano hayo yanadaiwa yaliendelea hadi mapema leo asubuhi.Hata hivyo polisi haikuweza kuthibitisha ni watu wangapi waliojeruhiwa au kuuwawa kwenye ghasia hizo.

Mazungumzo yakutafuta maridhiano nchini humo yanasekana hayaleti tija yoyote na hali ya usalama inazidi kuzorota japo walioandaa mazungumzo yanayoendelea wanasema ni hatua kubwa kufanyika kwa mazungumzo hayo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com