1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mogadishu.Mamia kadha ya watu wauwawa.

30 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCf5

Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu limesema kuwa mamia kadha ya watu wameuwawa katika mapigano ya hivi karibuni nchini Somalia, na maelfu wengine wamelazimika kukimbia makaazi yao.

Wakati shirika la umoja wa mataifa la kuwahudumia wakimbizi limeonya kuwa wimbi kubwa la wakimbizi litamiminika katika mataifa jirani, shirika la msalaba mwekundu limesema hakuna wakimbizi waliokuwa wakikimbia kutoka Somalia.

Shirika hilo limesema badala yake watu wanarejea katika mji mkuu. Mapema siku ya Ijumaa waziri mkuu wa Somalia Ali Mohamed Gedi aliingia mjini Mogadishu akishangiliwa na makundi ya watu, siku moja baada ya majeshi yanayosadiwa na Ethiopia yalipowaondoa wapiganaji wa mahakama za Kiislamu kutoka katika mji huo.