1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU:Bomu la kutegwa barabarani laripuka

6 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBlH

Takriban watu sita wameuawa hii leo wakati bomu la kutegwa barabarani lililporipuka mjini Mogadishu.Tukio hilo linafanyika ikiwa ni wiki moja kabla kufunguliwa rasmi kwa mkutano wa kutafuta amani ulioahirishwa mara tatu.

Mlipuko huo ulitokea katika eneo la Suuqaholaha kaskazini mwa Mogadishu ulisababisha watu 7 kujeruhiwa.

Milipuko ya mabomu ya kutegwa barabarani,maguruneti na hata mashambulio ya risasi yanazidi kutokea mjini Mogadishu tangu jeshi la Somalia linaloungwa mkono na majeshi ya Ethiopia kuwafurusha wapiganaji wa mahakama za kiislamu mwezi Aprili baada ya muda wa miezi mingi ya mapigano.

Mashambulio hayo pamoja na uhaba wa fedha vimesababisha mkutano unaoandaliwa na serikali kuahirishwa mara tatu.Kikao hicho kinapangwa kufanyika tarehe 15 mwezi huu.Nchi ya Somali imekuwa bila serikali maalum tangu kungolewa madarakani kwa Siad Barre mwaka 91.