MOGADISHU: Watu wasiopungua 10 wauwawa | Habari za Ulimwengu | DW | 28.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOGADISHU: Watu wasiopungua 10 wauwawa

Watu wasiopungua 10 wameuwawa kwenye mapigano makali yaliyozuka mjini Mogadishu nchini Somalia kati ya wanajeshi wa Ethiopia na wapiganaji wa kisomali.

Walioshuhudia wanasema watu hao waliuwawa kwenye ufyatulianaji wa risasi na mashambulizi ya makombora wakati wanajeshi wa Ethiopia walipokuwa wakifanya operesheni dhidi ya wapiganaji wa kisomali mjini Mogadishu.

Somalia imekabiliwa na ongezeko kubwa la machafuko tangu wanajeshi wa serikali ya mpito wakisaidiwa na wanajeshi wa Ethiopia walipofaulu kuwafukuza wanamgambo wa kiislamu kutoka Mogadishu mwezi Disemba mwaka jana.

Mamia ya raia wameuwawa katika mapigano nchini Somalia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com