1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU : Wanane wauwawa katika machafuko mapya

10 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7H1

Raia wanane wa Somalia wameuwawa katika machafuko mapya nchini Somalia na waziri mkuu wa nchi hiyo amekuwa akipigania kubakia madarakani kabla ya kupigwa kura ya kutokuwa na imani naye baadae wiki hii.

Umwagaji damu mpya kwenye mji wa Mogadishu ulianza jana usiku wakati wapiganaji waasi waliposhambulia kituo cha polisi. Mapigano yaliofuatia hapo yameuwa watu sita wakati mripuko mwengine wa bomu kwenye mji wa bandari wa Kismayo umeuwa watu wawili.

Wakati hayo yakitendeka Waziri Mkuu Ali M ohamed Gedi amekuwa akikutana na wafuasi wake huku kukiwepo repoti kwamba Rais Abdulaye Yusuf anataka kushinikiza kura ya kutokuwa na imani na serikali wiki hii na kuunda serikali mpya.