MOGADISHU: Wanajeshi wa Somalia wajiandaa kwa mashambulio ya wanamgambo | Habari za Ulimwengu | DW | 25.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOGADISHU: Wanajeshi wa Somalia wajiandaa kwa mashambulio ya wanamgambo

Wanajeshi wa Somalia wakisaidiwa na wanajeshi wa Ethioppia leo wameanaza kuchimba mitaro kwenye lango la makao makuu ya serikali ya mpito ya Somalia mjini Baidoa, kusini mwa nchi hiyo.

Walioshuhuduia wanasema hatua hiyo inafuatia hofu ya kufanywa shambulio na wapiganaji wa mahakama za kiislamu.

Akizungumza katika redio ya HornAfrik hii leo, afisa wa mahakama za kiislamu, Hassan Turki, amesema wanapania kuushambulia mji wa Baidoa. Aidha amesema mahakama za kiislamu zinataka kupanua eneo la utawala wake lakini hakutoa maelezo ya kina.

Katika kipindi cha miezi mitano iliyopita, mahakama za kiislamu zimeyateka maeneo mengi ya kusini mwa Somalia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com