MOGADISHU: Waasi washambulia kituo cha polisi | Habari za Ulimwengu | DW | 29.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOGADISHU: Waasi washambulia kituo cha polisi

Nchini Somalia,hadi raia 4 wameuawa katika mashambulizi makali yaliyofanywa na waasi dhidi ya kituo cha polisi kusini ya mji mkuu,Mogadishu. Wanamgambo wenye silaha nzito,Ijumaa usiku walivamia na kukidhibiti kituo hicho cha polisi kwa muda mfupi,katika mashambulizi makubwa kupata kufanywa dhidi ya stesheni ya polisi tangu serikali kuhamia mjini Mogadishu.

Mashambulizi ya kila siku mjini Mogadishu yameongezeka,tangu kundi la upinzani lililoundwa nchini Eritrea mapema mwezi huu kula kiapo kuwa litavishinda vikosi vya Ethiopia vilivyokuwepo nchini Somalia.Mwaka jana,vikosi vya serikali kwa msaada wa majeshi ya Ethiopia viliwatimua wanamgambo wa Kiislamu waliokuwa wakidhibiti sehemu nyingi nchini Somalia.Nchi hiyo kwenye Pembe ya Afrika haina serikali kuu tangu kupinduliwa kwa dikteta Mohamed Siad Barre mnamo mwaka 1991.Juhudi nyingi za kutaka kurejesha utulivu na amani hadi hivi sasa hazikufanikiwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com