1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Mwanajeshi wa Uganda auwawa

1 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCDO

Mwanajeshi mmoja wa Uganda ameuwawa kwenye mapigano yanayoendelea mjini Mogadishu nchini Somalia. Kifo cha mwanajeshi huyo ni cha kwanza cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika wanaolinda amani nchini humo.

Msemaji wa jeshi la Uganda, meja Felix Kulaije, amesema wanajeshi wa Uganda walikuwa wakiilinda ikulu ya rais wa serikali ya mpito ya Somalia hapo jana wakati waliposhambuliwa na maroketi. Mwanajeshi mmoja aliuwawa na wengine watano kujeruhiwa.

Mapigano mjini Mogadishu yamesababisha uharibifu mkubwa huku yakiingia siku yake ya nne hii leo.

Wakaazi wanaoishi karibu na uwanja mkubwa wa kandanda mjini Mogadishu na kitongoji cha Ali Kamin, ambako wanamgambo wa kiislamu wanaendelea kupambana na majeshi ya serikali ya mpito ya Somalia yakisaidiwa na majeshi ya Ethiopia, wanayahama makazi yao.